Baada ya mateso ya muda mrefu ya uwashaji moto wa mkaa kwa njia mbalimbali kama kwa kutumia magunzi, ndala chakavu, vifungashio vya nailoni, Ceiling Board chakavu au vikuni vidogo vidogo hatimaye SULUHISHO la uwashaji moto limepatikana na kuleta tabasamu katika familia nyingi nchini, Hii ni mijini na Vijijini.
Kuingizwa sokoni kwa VIJITI vya KUWASHIA MOTO kumeokoa muda uliokuwa unapotea kwa kupambana kutafuta viwashio vya moto ambavyo vitauwasha kwa muda mfupi lakini ilikuwa haiwezekani. Vijiti hivi vimeokoa muda sasa kwani hivi sasa moto unawashwa kwa dakika tano tu mkaa unakuwa umekolea.
Lakini umewahi kujiuliza VIJITI HIVI vinatokana na nini?
Basi kaa kwa kutulia nami nitakueleza leo ni mti gani huzalisha VIJITI hivyo.
Wengi wetu bila shaka mmewahi kuusikia mti wa mbao uitwao MPAINA almaarufu kama MSINDANO, Kwa watu wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa miti hii si migeni kwao kwani ni moja ya miti inayotoa mbao kwa wingi na ni mti unaopandwa na si wa asili kama ilivyo miti ya Mninga.
MPAINA unatoaje VIJITI VYA KUWASHIA MOTO?
Baada ya kukata miti kwa ajili ya mbao kutoka kwenye MIPAINA hiyo kuna visiki ambavyo husalia.
Visiki hivyo vilivyosalia baada ya miti ya mbao kutolewa huanza kutengeneza mafuta taratibu kwa kipindi kirefu. Na Kumbuka kuwa miti hiyo ni ile ambayo imekomaa vizuri si kila Mpaina unatoa vijiti hivyo. Ni ile tu ambayo imekomaa vizuri na kukaa kwa muda mrefu katika hali hiyo ya Visiki. Baada hapo Visiki hivyo huwa tayari kwa mavuno ya Vimiti ambavyo hupasuliwa na kutengeneza vijiti hivyo vya moto.
VIJITI hivi vinazalishwa kwa wingi katika maeneo ya MAFINGA mkoani IRINGA, wilayani MAKETE na katika mkoa wa MBEYA ndani ya wilaya za RUNGWE (Tukuyu), BUSOKELO na MBEYA VIJIJINI. Kwa wafanyabiashara wa mikoani ambao mnahitaji BIDHAA HII YA VIJITI mnaweza kuwasiliana na mimi kwa namba hizo hapo kwenye picha au 0743204194 (whatsApp) kwa wale wanaohitaji mzigo wa jumla tutakuuzia kwa bei rahisi sana.
Karibuni sana tufanye biashara hii ambayo ina soko kila kona ya Tanzania kwa sasa.