Uongozi wa Timu ya soka ya Azam kutoka Chamazi jijini Dar es Salaam imethibitisha kupokea OFA mbili kutoka kwa timu za Simba ya Tanzania na Al Hilal ya Sudan. OFA hizo zimekuja mezani kwao kwa pamoja zikihitaji huduma ya Mchezaji wao Prince Dube ambaye hivi karibuni aliomba kuvunja mkataba.
Pamoja na timu hizo kutuma OFA zao Uongozi wa timu hiyo umebainisha kuwa unaendelea kupitia moja baada ya nyingine kuona ni ipi yenye manufaa kwao huku wakizikaribisha na timu nyingine kuleta OFA zao kwani milango haijafungwa.
Tags:
Sports