PADRE AIBA HUNDI YA FEDHA YA MUUMINI WAKE

 


INASIKITISHA SANA


Jinsi Padre Alivyoiba hundi(cheque) ya Benki ya $ 25,000.00 Wakati wa Chakula cha jioni katika Nyumba ya muumini wake


Wanandoa katika Parokia fulani walimwalika baba Paroko wa Parokia yao kwa chakula cha jioni nyumbani kwao. Paroko alifurahi sana na alipomaliza kula aliwaaga kisha  akaenda zake parokiani anakosishi.


Ila Baada ya Paroko kuondoka, wenzi hao waligundua hundi(cheque) yao imepotea. Mtu huyo alimwambia mkewe; "Nadhani Mchungaji ameiba hundi ya benki iliyo wazi ya $ 25,000.00 ambayo niliiweka hapa kwenye meza ambayo nilikuwa na nia ya kumpa".


Kwa hasira mkewe akasema; “Hmmmm! Kumbe watu wote ni sawa tu. Ikiwa ni wezi, au matapeli, hakuna haja ya kumwalika tena, tokea sasa tutahudhuria Kanisa lingine ”.


Miezi miwili Baadaye, mwanamke huyo alikutana na Paroko wake  kwenye barabara fulani, na alikuwa na ujasiri wa kutosha kumkabili na akasema: “Habari za asubuhi baba Paroko, umegundua kuwa hatuji Kanisani tena eeeh?, hii ni kwa sababu tumekukasirikia. Ile Siku tuliyo kualika kuja kula chakula nyumbani kwetu, pale mezani kulikuwa na hundi ya benki ya $25,000.00 lakini kwa bahati mbaya ilipotea wakati tunakula. Wewe ndiye mtu pekee uliyefika nyumba kwetu  siku ile”.


Baba Paroko akamwambia, “Ndiyo, ni kweli niliichukua hundi hiyo nikaiweka ndani ya Biblia yako ili kuepuka kuimwagia mchuzi ”.


Mwanamke huyo alichanganyikiwa sana na akalia huku akimsihi  baba Paroko amsamehe.


Kurudi nyumbani kwake, alichukua Biblia na kuipekua akaipata hundi ya benki ambayo ilikuwa imekaa kwa miezi miwili.


Hii ilimaanisha kuwa kwa miezi miwili, alikuwa hajaifungua biblia yake. Kwa miezi miwili, yeye na mumewe walimshtaki baba Paroko asiye na hatia. Kwa miezi miwili, tukio hilo lilikuwa likiwatesa bila sababu.


Ni mara ngapi tunashuku na kuwashitaki watu wengine bila uthibitisho wa kweli, ushahidi au ushuhuda?


Ni mara ngapi unampa mtu jina baya ?


Ni mara ngapi unatafsiri vibaya matendo ya kaka au dada ambayo wao walikua hawana nia mbaya  kwako?


*Somo*: ikiwa unafikiria ndugu yako  amekukosea..mwambie .... muulize ... Mrekebishane kwa upendo.... usiweke kinyongo  cha bure, kwa kumhisi mtu kwa jambo ambalo hana hatia nalo.

Hisia ni mbaya sana.


Washirikishe wengine hadithi hii yenye mafunzo. Umebarikiwa

Asante sana


SHUKRANI ZA PEKEE KWA MTUNZI WA SOMO HILI POPOTE ALIPO.

Imetolewa kwenye Group za WhatsApp. 

Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post