HADITHI: ZAWADI YA UPENDO - 05 (MTUNZI HADIJA S. MGAZA)

 ZAWADI YA UPENDO 

MTUNZI: Hadija Mgaza 

Episode 05

WhatsApp..no.0678204094


Tuendelee tulipoishia katika sehemu ya Nne ya Simulizi hii.... 

Adnani nae alirudi. Na kumkuta mkewe anatapika Tena 

"Wewe vipi Tena ?" 

"Ata sijui kwa Nini" 

"Embu twende dispensary ukapime ..." 

"Aahaaa saizi jamani ..." 

"Sitaki kusikia , Yani unatapika hivi kweli 

Aaah hapana kwa kweli twende tuka..." 

"Lakini Mimi sijisikii kuumwa." 

" Uwe unaumwa au hauumwi twende .inatakiwa twende tu .. kwasababu unatapika Sana." 

"Sawa ngoja ninawe hata miguu .." 

"Hakuna kunawa." 

"Jamani." 

"Hakuna Cha jamani hapa." 

Basi Adnani alimshika mkono mkewe na kutoka nnje..

"Mama tuna toka kidogo." 

Mama alikua kimyaa tu hakujibu

"Mmmh.. mmewangu . Kwani umefanyeje mama ?" 

"Wala sijamfanya kitu mie.." 

"Mbona hataki ata kujibu kwanini?" 

"Mi mwenyewe sijui ..kwanza asikuumize kichwa. Yule Ni mtu mzima anajua anacho kifanya." 

Adnani na mkewe wakaenda huko kupima afya yake..

Walifika vizuri na hawaja kaa mda mrefu saana ..wakapima na munira aliambiwa anaujauzito ...Walifurahi Sana 

"Mkewangu inamaana kweli nataka kuitwa baba ...?" 

"Jamani hata Mimi nataka kuitwa mama .....! Ee mungu Yani Nina furaha mpaka namkumbuka baba ..." 

"Mmmh..hata Mimi namkumbuka baba ..." 

Basi wakacheka kwa pamoja ..

Walielekea nyumbani ..huku wakiwa na furaha ...

Walifika na kupitiliza moja kwa moja chumbani..

"Mkewangu inamaana ulikua hujui Kama una ujauzito .?" 

"Mi sijui bwana ..we mwenye unajua ..naweza kukaa ha miezi mitatu siingii mwenzini ..we unafikili nitajuaje .." 

"Ila Mimi nilijua ...🥰" 

"Mmmh..muongo ...wewe sa mbona hukunambia ?" 

"Mmmh..ulitaka nikwambie kwanini ?" 

"Hahahàaa wewe Ni muongo Sana ..." 

Huku mlangoni mama na mtoto  wake zuhura baada ya kusikia kicheko Cha chumbani. 

"Mmmh..mama Yani wenzetu wanafuraha hivi .. halafu sisi tumetulia tu..." 

"Yani roho inaniuma kweli, embu ngoja nigonge ..." 

Mara akatokea Zahara ...

"Kheee nyie kuna nini ?" 

"Khoo kivuruge kasha fika tayari maana huyu mama wakuharibu mambo .." 

"Kimyaaa ..wewe nyoooo ..kazi umbea tu ..." 

"Mama hivi nyinyi mnashida gani lakini, Mama mnakaa mlangoni kwa Kaka ..? Mama hiyo Ni tabia mbaya kwanini lakini mnatia aibu ?" 

"He he heee wewe ..kwaiyo wewe kupata marafiki wa mjini tayari ..Usha badirika ?" 

"Sio kubadirika mama ...tatizo hili mnaro litenda Ni sawa ..haya Sasa hapo mliko kaa mnasikiliza vya ndani ..kwani nyinyi Ni wake weza wa munira?" 

"Unasemaje wewe? yani unatutusi.." 

Mama aliongea huku akimfata Zahara kwa Kasi akifatiwa na zuhura, Wakamshika na kuanza kumpiga. Zahara akaanza kupiga kelele ...

"Kaka nakufaa Kaka nakufaa..😭" 

 "Mume wangu mbona nasikia kelele huko nnje .." 

"Hata Mimi nasikia ...embu nisubiri nikaangalie ..." 

"Mmm lakini hiyo Ni sauti ya Zahara .. sijui Nini kimetokea jamani." 

"Aaaa we tulia apo." 

"Kwanini nikae ..!?" 

"Wewe Ni mjamzito .." 

"We nawe sa Kuna ubaya gani ?Embu twende huko." 

"Katoto kabishi hakaaa..." 

Alisema Adnani huku akimshika mkono mkewe, Walifika nnje na kukuta mama ana mpiga Zahara na kiatu. 

"Mama vipi ?" 

Mama akawa kimya huku anaendelea kumpiga ..

Adnani akaenda kumzuiya mama yake..

"Mama ..mbona mnakua hivi lakini ..kwani amekosa Nini mpaka umpige hivyo, Halafu mama Zahara Ni mtu mzima ..." 

"Kwaiyo unanifundisha au? ...embu kwenda ..ukifanya ujinga hata wewe nakichapa.." 

Mama alipngea huku akiondoka ..

"Nyanyuka kwanza wifi yangu .." 

Alisema munira huku akimsaidia kunyanyuka ...

"Zahara kwani umemkosea Nini mama lakini ..halafu mtu mwenyewe unamjua akili zake .." 

"Kaka mi sijakosea chochote ..." 

Zuhura alivyo ona Zahara anataka kuongea aliamua kuondoka. 

"Kama huja mkosea kakupigia Nini ?" 

"Kaka na wifi ..kusema ukweli, Mambo wanayo fanya mama na dada sipendi kabisa ..kipindi mi natoka zangu ..nikawakuta mama na da zuu wapo mlangoni kweni wamesimama ..Yani Kama wanasikiliza kitu vile .." 

"Wewe embu rudia Tena ..Yani unamaanisha kwenye mlango wangu Mimi na mkewangu au?" 

"Ndio Kaka ..." 

Adnani na mkewe waliangaliana kwanza ..

"Yani mlango wetu sisi ..?" 

"Ndio ..sa mimi nikawa nawauliza kwanini wamekaa pale ..Waka kasirika na kuja kunipiga ..." 

Adnani alichoka hoi ..

"Mkewangu naomba unisamehe Mimi ..lakini mama wanaondoka leo.." 

"Hapana mume wangu kipenzi naomba usichukue maamuzi ukiwa na hasira .." 

"Hapana mkewangu ..huruma yako ndo inakuponza ..mi naenda mfukuza .." 

"Mi ni mkeo naomba uheshimu maamuzi yangu ..Yule Ni mama huwezi kumfukuza .." 

"Mkewangu ..mama ananifanya nijisikie aibu yani nakuonea aibu mkewangu ..huyu Ni mama wa aina gani Sasa aaaa...." 

Alisema Adnani na kuondoka 

"Wifi yangu naomba unisamehe ..mi nimesema ukweli tu, Lakini wifi yangu mungu akubariki Sana ..una moyo wa kipekee Sana ..sema ndugu zangu hawalijui Hilo ..." 

"Zahara nenda kaoge kwanza maana una mavumbi kweli ..ngoja niende nikamuangalie kaka yako." 


Nini kitaendelea? Tukutane katika sehemu inayofuata ya simulizi hii ya ZAWADI YA UPENDO.




Sultan Uwezo

In our hands you will find out Songs and Videos of Various Artists without forgetting News from Newspapers. Here you will also find Employment's Information from the Government and the Private Sectors.

Post a Comment

Previous Post Next Post